Monday, August 22, 2016

Published August 22, 2016 by with 0 comment

Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza kukamatwa watu wote watakaobainika kuwarubuni watoto wa kike




Screen Shot 2016-08-22 at 3.37.35 PM
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria watu wote watakaobainika kuwarubuni watoto wa kike kwa kuwapa ujauzito wakiwa shuleni.
Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Katavi  ,Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Azimio vilivypo Manispaa ya Mpanda mkoani  humo.
Katika Mkutano huo,Waziri Mkuu alipokelewa na umati mkubwa wa watu, huku wengine wakiwa wamebeba mabango mbalimbali ya kufikisha ujumbe wa kero walizonazo wananchi ikiwemo kukithiri migogoro ya ardhi, ujenzi wa viwanda kwenye makazi pamoja na madai kuliwa fedha za michango ya Saccos ya Walimu.
Akihutubia mkutano huo, licha ya kukemea tabia ya baadhi ya watu kutojali maendeleo ya mtoto wa kike, hali inayorudisha nyuma maendeleo yao kielimu,Waziri Mkuu pia alitoa tahadhari kwa watumishi wa umma kutumia vyema fedha zinazoletwa na Serikali, ikiwemo  Mapato ya Halmashauri katika Shughuli za Maendeleo.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameitaka Halmashauri ya Mpanda, kupitia Mweka Hazina wa Manispaa hiyo, kuwasilisha haraka iwezekanavyo michango ya Saccos ya Walimu.
Akizungumza katika mkutano huo, Mbunge wa Mpanda Mjini 
Sebastian Kapufi amebainisha changamoto za jimbo hilo ikiwemo waendesha Bodaboda kutumia gharama kubwa ya kupata leseni.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu pia ametembelea eneo la hifadhi ya wakimbizi waliopatiwa uraia katika kambi ya Katumba, Halmashauri ya
Nsimbo na Hospitali ya wilaya.

      edit

0 comments:

Post a Comment