Majambazi watatu wameuwawa jijini Dsm huku mmoja wao katika eneo la mabibo na kukutwa na Magazini kumi zenye risasi mia 300 za Bunduki aina ya SMG pamoja na bomu huku majambazi wengine wanne wakitoroka baada ya kurusha bomu la mkono.
Kamishna wa Polisi kanda Maalum dsm CP Simon siro amesema tukio hilo limetokea alfajiri ya kuamkia leo ambapo vijana wapatao hamsini waliwaitilia mashaka watu watano waliokuwa wamebeba mabegi ambayo ndani yake kulikuwa na silaha.
Jeshi hilo limeanzisha msako mkali dhidi ya majambazi wengine wanne wanaosadikiwa kuwa na bunduki za SMG na kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa ili kufanikishwa kutiwa mbaroni kwa majambazi hao.
Katika tukio lingine kinara wa wizi wa vifaa vya magari Salum Issa Hassan mfabiashara eneo la kariakoo anashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukutwa na vifaa vya wizi vilivyoibwa katika magari zaidi ya 300 zikiwemo,sight Milla,taa.Vioo pamoja na Vitasa vya magari.
Katika kukabiliana na tishio la Operesheni Ukuta jeshi hilo limefanikiwa kumkamata mfanyabiashara Yoram Sethy Mbyela akiwa na fulana zaidi ya 200 zenye maneno ya Uchochezi kuhamasisha maandamano ya Ukuta na Hapa anatoa onyo.

0 comments:
Post a Comment