Thursday, October 26, 2017

Published October 26, 2017 by with 0 comment

Kukatika umeme kwaweka rehani ajira za mabosi Tanesco

Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amemtaka Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Abdallah Ikwasa kumuondoa mara moja meneja uendeshaji wa kituo cha umeme  Kidatu akituhumiwa kwa uzembe.

Dk Kalemani amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 baada ya kukosekana umeme nchi nzima jana Jumatano Oktoba 25,2017 kwa takriban saa 10, huku kukiwa hakuna ufafanuzi wa kueleweka.

Waziri amemtaka meneja huyo kuandika barua ya kujieleza ndani ya saa tatu ni kwa nini asiondolewe katika nafasi hiyo.

Dk Kalemani pia amempa siku tatu Meneja Udhibiti wa Mitambo, Mhandisi Izihaki Mosha kujieleza ni kwa nini anastahili kubaki katika nafasi hiyo.

Mbali na maagizo hayo, waziri amemtaka Ikwasa; Naibu Mkurugenzi Usafirishaji, Mhandisi Bishaija Kahitwa na Mosha kuandika barua za kuachia nafasi zao iwapo umeme hautarudi siku nzima leo.

“Siwaondoi, bali nataka umeme usiporudi muondoke wenyewe katika nafsi zenu kwa sababu hii kazi itakuwa imewashinda,” amesema.

Dk Kalemani amesema, “Haiwezekani umeme ukatike nchi nzima ndani ya saa 10 na bado hamjajua tatizo ni nini, wananchi wanatuma ujumbe mfupi kila kona wameunguliwa vitu vyao, wameunguliwa mashine zao nani atalipa hizo gharama.”

Waziri aliyefanya ziara kwenye mitambo ya kuzalisha umeme Ubungo na Kinyerezi I jijini Dar es Salaam kubaini chanzo cha kukatika kwa umeme nchi nzima, amesema wakati wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha.

Amesema haiwezekani kusiwe na spea za akiba za mitambo ambayo ni muhimu katika uzalishaji wa umeme.

Dk Kalemani amehoji iwapo kulikuwa na hitilafu kwenye gridi ya Taifa ni kwa nini mashine nyingine nazo zipoteze mwelekeo huku kukiwa na kitengo cha mfumo wa uendeshaji.

“Hakuna haja ya kuwa na mfumo ambao hautoi taarifa mapema kama kuna tukio hatarishi linakuja, ninachotaka kusikia ni nini kifanyike ili tuwe na taarifa mapema,” amesema.

Waziri amesema, “Kila mnaloulizwa hamjui, mnasubiri hadi mitambo iharibike ndipo mchukue hatua, nchi haiwezi kuendeshwa hivyo, kukosa umeme ndani ya saa 10 ni hatari kwa mali za raia lakini kwa usalama pia. ”

“Sitaki kubishana hilo ndilo neno ninalowaacha nalo leo, nataka umeme urudi nchi nzima, hii haiwezekani,” amesema Dk Kalemani.

Pia, ameagiza mkandarasi anayeshughulikia mfumo wa utendaji wa umeme ambaye yupo nje ya nchi kurudi nchini.

“Nataka awepo kazini kesho na sitaondoka kuelekea Dodoma hadi nijue hatima ya mkandarasi, ” amesema.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Mwakyembe Amteua Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Waziri wa Habari Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amemchagua Mwanasheria na mdau wa masuala ya Sanaa Alberto Msando kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki.

Katika tarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi Leah Kihimbi kuhusu uteuzi huo wa Msando imesema kwamba uteuzi huo umetokana na vikao vilivyofanywa na wadau wa sanaa pamoja Mh. Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wa Alberto Msando ambaye amepatiwa nafasi hiyo na serikali ameahidi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria za nchi zinalinda haki za wasanii na kuhakikisha wasanii wanafaidika na kazi zao.

Msando ameandika  "Ulaya na Marekani wasanii wengi sio masikini. Hapa kwetu wasanii wengi ni majina tu. Wengi wanaishi maisha ya 'naomba nitoe niko vibaya'. ni wakati sasa wa kuhakikisha sheria zetu zinalinda haki za wasanii".

Ameongeza "Harrison Mwakyembe tutafanya kazi uliyotutuma"

Msando mara nyingi amekuwa mbele katika kuwasaidia wasanii kwenye masuala yanayohitaji msaada wa kisheria.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Wanafunzi 21,000 wapangiwa mkopo elimu ya juu

Kiasi cha Sh72.2 bilioni mpaka sasa kimetolewa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 21,677 kati ya wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza waliopangwa kupatiwa mikopo yenye thamani ya Sh 108.8 bilioni kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru imesema kuwa idadi ya wanafunzi waliobaki wapatao 8,323 watapangiwa mikopo yenye thamani ya Sh 36.6 bilioni katika awamu inayofuata ili kukamilisha idadi iliyopangwa.

“Idadi ya wanafunzi 21,677 waliokwishapangiwa mikopo na ambao wamedahiliwa katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu vinavyotambulika ni asilimia 72.2 ya wanafunzi 30,000 wanaotarajiwa kunufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018,” imesema taarifa hiyo

Orodha ya majina ya wanafunzi hao 21,677 inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz na itatumwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya hatua zaidi za kukamilisha malipo ya mikopo.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Lulu Michael akutwa na hatia ya kuua bila kukusudia, hukumu yake kutolewa Novemba 13

Kesi inayomkabili muigizaji wa Filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo alhamisi imeendelea kusikilizwa Mahakamani ambapo washauri watatu wa Mahakama kuu wamesema mshitakiwa Lulu aliua bila ya kukusudia.

Baada ya kusikiliza maoni ya baraza la wazee leo Mahakama kuu ya tanzania, imesema Elizabeth Michael amekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia, muigizaji mwenzake Steven Kanumba ambaye alikuwa mpenzi wake na hukumu yake itatolewa Novemba 13.

Wazee hao ambao walikuwa watatu, kila mmoja alitoa maoni yake na kusema kwamba muigizaji huyo ana hatia ya kuua bila kukusudia, kwani marehemu alikuwa na mwili mkubwa zaidi ya mshtakiwa.

Kabla ya  wazee kutoa maoni, Jaji Rumanyika ambaye ndiye anayeendesha kesi hiyo, alisoma maelezo ya ushahidi wa pande zote mbili na kusema kwamba ushahidi upande wa mashtaka umejikita katika ushahidi wa kimazingira kwa kuwa Lulu ndiye mtu wa mwisho kuwa na Kanumba, kisha kusikiliza maoni hayo.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Novemba 13, ambapo hukumu yake itasomwa.

Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Ushahidi wa awali kwa watuhumiwa wawili wa kulawiti watoto 14 mkoani Singida Daud Idd na Abdallah Yahaya tayari umewasilishwa kwa mwanasheria wa serikali

Ushahidi wa awali kwa watuhumiwa wawili wa  kulawiti watoto 14 mkoani Singida Daud Idd na Abdallah Yahaya tayari umewasilishwa kwa mwanasheria wa serikali kanda ya Singida ili kuweza kuandaa hati ya mashtaka.

Hilo limethibitishwa na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Mratibu Mwandamizi wa Polisi Costantine ambaye amesema hatua za awali za kufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walalamikaji ambao ni wazazi wa watoto, umekamilika na kinachosubiriwa ni Mwanasheria kuandaa hati ya mashtaka.

“Tayari jeshi la polisi limeshakusanya ushahidi na kuukabidhi kwa mwanasheria wa serikali kanda ya Singida ili aupitie na akiridhika nao kwamba unajitosheleza kwaajili ya watuhumiwa kufunguliwa kesi basi mara moja watuhumiwa watafikishwa mahakamani”, amesema Kamanda Costantine.

Daudi Idd (74) ambaye ni mganga wa kienyeji pamoja na Abdallah Yahaya (31) ambaye ni mtoto wa mdogo wake wanadaiwa kuwalawiti na kuwabaka watoto 14 kwa nyakati tofauti kati ya Disemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.

Watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 16 mwaka huu baada ya mtoto mmoja wa miaka 7 kulalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri alipokuwa akiogeshwa na mama yake ndipo mama huyo akachunguza na kubaini kuna michubuko inayotokana na kuingiliwa kimwili ndipo akaripoti Polisi.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Octoba 26

      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Bashe Awanyooshea Kidole Polisi

Mbunge wa Jimbo la Nzega kwa tiketi ya (CCM) Hussein Mohammed Bashe amefunguka na kusema zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa kijiji cha Undomo kilichopo Kata ya Uchama Nzega wamehama makazi yao kutokana na kamata kamata inayofanya na jeshi la polisi.

Bashe amesema hayo baada ya jana kufanikiwa kuzitembelea familia tano ambazo zimeathirika kutokana na imani za kishirikina ambapo kina mama watano walipigwa na kuchomwa moto na wanakijiji wakituhumiwa kuwa ni wachawi, kufuatia jambo hilo jeshi la polisi liliweza kukamata watu zaidi ya 60 na kuligeuza tukio hilo kama njia ya kujipatia kipato jambo ambalo Mbunge anasema halikubaliki.

"Kina mama watano walipigwa na kuchomwa moto kwa kuwa walituhumiwa kuwa ni wachawi, jeshi la polisi lilikamata watu zaidi ya 60 na uchunguzi unaendelea, jambo jingine ambalo limejitokeza wakazi zaidi ya asilimia 60 wamehama na kufunga nyumba zao kwakua jeshi la polisi limegeuza tukio hilo mradi na kila mtu ambae anakipato hukamatwa na kutakiwa atoe rushwa ama asipotoa anaunganishwa katika kesi jambo hili nimelifikisha kwa mamlaka husika" alisema Bashe

Mbunge Hussein Bashe akiwa na familia ya Katekista ambae mke wake alichomwa moto na watu wasiokua na utu wala ubinadamu katika kijiji hicho.

Aidha Mbunge Bashe amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na jeshi la polisi ili wale waliohusika kweli kwenye tukio hilo waadhibiwe ila wale ambao hawahusiki na wamekamatwa wasigeuzwe chanzo cha mapato kwa askari wa polisi na jeshi hilo.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Katibu Mkuu CHADEMA Atakiwa Kuripoti Polisi

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ametakiwa kuripoti ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imeelezwa.

Dk Mashinji anakwenda kuripoti kipindi ambacho Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa chama hicho, Kigaila Benson anaendelea kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Mwanasheria wa Chadema, Fredrick Kihwelo amesema, “Katibu Mkuu ametakiwa kuripoti kwa DCI na sasa natoka hapa Central kwa Kigaila nakwenda huko."

Amesema suala la Kigaila kupata dhamana au kupelekwa mahakamani litajulikana mchana wa leo baada ya kutakiwa kurudi Kituo Kikuu cha Polisi.

Kihwelo alipoulizwa ni nini sababu ya Dk Mashinji kuitwa kwa DCI, amesema itakuwa ni mwendelezo wa mahojiano na Jeshi la Polisi kuhusu tuhuma za kutoa lugha za uchochezi alipozungumzia hali ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Kigaila ambaye ameshafikisha saa 72 akiwa rumande tangu alipojisalimisha kituoni hapo Jumatatu Oktoba 23,2017 na kuhojiwa kwa kutoa lugha za uchochezi katika mkutano na wanahabari Oktoba 12,2017 makao makuu ya Chadema wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Faili la Mganga Aliyebaka watoto 14 Lakabidhiwa kwa Mwanasheria wa Serikali

Ushahidi wa awali kwa watuhumiwa wawili wa  kulawiti watoto 14 mkoani Singida Daud Idd na Abdallah Yahaya tayari umewasilishwa kwa mwanasheria wa serikali kanda ya Singida ili kuweza kuandaa hati ya mashtaka.

Hilo limethibitishwa na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Mratibu Mwandamizi wa Polisi Costantine ambaye amesema hatua za awali za kufanya uchunguzi baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa walalamikaji ambao ni wazazi wa watoto, umekamilika na kinachosubiriwa ni Mwanasheria kuandaa hati ya mashtaka.

“Tayari jeshi la polisi limeshakusanya ushahidi na kuukabidhi kwa mwanasheria wa serikali kanda ya Singida ili aupitie na akiridhika nao kwamba unajitosheleza kwaajili ya watuhumiwa kufunguliwa kesi basi mara moja watuhumiwa watafikishwa mahakamani”, amesema Kamanda Costantine.

Daudi Idd (74) ambaye ni mganga wa kienyeji pamoja na Abdallah Yahaya (31) ambaye ni mtoto wa mdogo wake wanadaiwa kuwalawiti na kuwabaka watoto 14 kwa nyakati tofauti kati ya Disemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.

Watuhumiwa hao walikamatwa Oktoba 16 mwaka huu baada ya mtoto mmoja wa miaka 7 kulalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri alipokuwa akiogeshwa na mama yake ndipo mama huyo akachunguza na kubaini kuna michubuko inayotokana na kuingiliwa kimwili ndipo akaripoti Polisi.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Mkurugenzi NEC: Matokeo ya Rais Hayawezi Kuhojiwa Popote, Labda Tubadili Katiba

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Kailima Ramadhani, amesema kitendo cha kuweza kushtaki mahakamani na kupinga matokeo ya urais kama ilivyofanyika Kenya, nchini Tanzania haitawezekana kutokana na sheria zake za uchaguzi.

Kailima ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba sheria za Kenya zinaruhusu jambo hilo, lakini hapa kwetu litawezekana tu iwapo katiba ya nchi itabadilishwa.

“Wao wametekeleza ile kazi kwa mujibu wa sheria za Kenya, na sisi tunatekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria zetu, huwezi kufanya kitu ambacho kwenye katiba yako hakuna, lakini kwa katiba ya Tanzania inasema matokeo ya Rais hayawezi kuhojiwa, kabadilishe katiba lete hilo jambo tutakwenda”, amesema Bwana Kailima.

Hivi karibuni Tanzania kunatarajiwa kufanyika chaguzi ndogo ndogo, kwa mujibu wa sheria za nchi na serikali za mitaa, ambazo pia zinasimamiwa na Tume ya Uchaguzi.
Read More
      edit
Published October 26, 2017 by with 0 comment

Waziri acharuka kuwekwa ndani watumishi wa afya


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekemea vitendo vya kuwaweka ndani watumishi wa afya bila kufuata utaratibu vinavyofanywa na wakuu wa wilaya na mikoa.

Amesema hayo leo Jumatano Oktoba 25,2017 katika kongamano la afya.

Mwalimu amesema makosa ya kitaaluma hayapaswi kumweka daktari au mtumishi wa afya ndani, bali anatakiwa kupelekwa kwenye baraza la madaktari.

"Juzi (Oktoba 23,2017) nimepigiwa simu daktari amewekwa ndani sababu mtoto amefariki dunia, nilishasema wakuu wa wilaya na mikoa msiingilie masuala ya utaalamu, wapelekeni baraza la madaktari. Ila akipatikana daktari amelewa, amepokea rushwa, mzembe awekwe ndani," amesema Mwalimu.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Obadia Nyongole amesema ni vyema Serikali ikaweka mfumo wa kuratibu utoaji huduma nchi nzima.
Read More
      edit