Sunday, February 4, 2018

Published February 04, 2018 by with 0 comment

Katambi Ataja Sababu Kuyumba Kwa Upinzani

 KADA mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ameeleza sababu zinazochangia kudhoofika kwa vyama vya upinzani nchini.

Amesema kuyumba kwa vyama hivyo kunachangiwa na ubinafsi waviongozi wake ambao wengine wamegeuza Chama ni mali yao na kutoa maamuzi ambayo si shirikishi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam January 2,Katambi alisema kuwa tangu ameondoka Chadema ambako alikuwa Mwenyekiti wa Vijana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amekuwa kimya muda mrefu lakini ameona ni vema akasema mambo kadhaa kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Kuhusu vyama vya siasa kuyumba, Katambi alisema zipo sababu ambazo zimekuwa zikichangia vyama hivyo kushindwa kuwa imara na matokeo yake kubaki kulalamikia kila jambo ambalo linafanywa na Serikali hata liwe lenye maslahi kwa nchi.

"Upinzani umeshindwa kujenga chama taasisi kwani hivi sasa kila chama ni cha mtu.Vyama vingi ni vya watu na si taasisi.Dhana ya taasisi ni kwamba sheria ,kanuni na taratibu lazima zifuatwe
"Kama mtu anadharau katiba na misingi iliyowekwa basi huo niudikteta. Wapinzani kabla ya kukimbilia kugombea udiwani na ubunge wajikite kwanza kujenga taasisi, kama wameshindwa kuheshimu katiba za vyama vyao wanapate uhalali wa kudai Katiba,"alisema.

Alisema sababu nyingine vyama vya upinzani vimekosa uamuzi shirikishi."Chadema ambayo inajieleza ni chama cha upinzani chenye nguvu kimeshindwa kuwa na utaratibu wa kuwa na maamuzi shirikishi na hata yanayoamriwa ni maamuzi ya mtu.Na pia kuna ukiukwaji wa uteuzi wa nafasi ikiwamo za ubunge viti maalumu ambao umetawaliwana rushwa  na kupeana nafasi kirafiki.

"Tatizo la upinzani hakuna kuheshimiana na ukosefu wa maadili ya viongozi. Kama Taifa lazima liwe na viongozi wanaozingatia maadili,kwa mfano leo hii Ukawa wakichukua nchi nani anaweza kuwa WaziriMkuu,"amesema.

Kada huyo wa CCM, amesema kuwa vyama vya upinzani adui yaomkubwa ni CCM lakini wameshindwa kuwa na uwazi kwenye mali zaokwani hata Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),akikagua ni lazima atapata hati zenye shaka kwani fedha za ruzukuzinatumika vibaya.

"Wanaosema nimenunuliwa wanajidanganya kwani wakati anakwenda chadema wamemnunua kwa shilingi ngapi. Kuna wabunge zaidi ya 15w ataondoka Chadema na kuna wajumbe wapo ndani ya chama hicho lakini tayari wameshaondoka ila wanaingia kwenye vikao ili kutimiza wajibu tu," alisema Katambi.

Alisema kwa sasa vyama vya upinzani wamekosa ajenda na waliopo huko  wanakwenda tu bora liende na wengine wanajua wakitoka hawataajirika.
"Kukosea ajenda chadema walikuwa wanasema wanapambana na ufisadi na hata Dr. slaa aligeukwa kwa sababu ya masilahi ya watu binafsi.Chadema ya Dk. Slaa kila mtu  anaifahamu ilifika wakati akapelekwa Marekani kwa ajili ya kuandaliwa ili aje kuwa Rais lakini baadaye wakaanza kumtuhumu kwa usaliti," alisema

Kutokana na hali hiyo amesema kuwa sasa umefika mwisho wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwani malengo ya Chadema yametimia kwa kuua nguvu ya kila chama ili wabaki wao katika upinzani.
Read More
      edit
Published February 04, 2018 by with 0 comment

Ratiba rasmi ya mazishi ya Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

Jumapili tarehe 4/2/2018
- Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street, Dar es salaam.

-Saa 11:00 Jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)

******************************
Jumatatu tarehe 5/2/2018
- Saa 1:00 Asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
- Saa 2:00 Asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
- Saa  4:00  Asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu
- Saa 6:00 Mchana mwili kuwasili Karimjee hall kwa shughuli ya kuagwa
- Saa 6:00 Mchana  9:00 Alasiri kuaga mwili wa marehemu
- Saa 9:00 Alasiri mpaka 9:30 Alasiri msafara wa kuelekea makaburini Kinondoni
- Saa 9:30  Alasiri mpaka 11:30 Jioni maziko
- Saa 11:30 Jioni 12:30 Jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu kwa chakula cha jioni kwa waombolezaji wote
1:30 mpaka  2:45  Usiku chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 Usiku-Hitimisho la shughuli ya Mzee wetu kwa waombolezaji wote.

Tunawashukuru sana waombolezaji wote kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu. Mungu awazidishie.

Bwana ametoa, na bwana ametwaa.
Jina lake na lihimidiwe - AMINA

Imetolewa na:
Omary A. Kimbau

Mwenyekiti wa kamati ya mazishi
Read More
      edit