Tuesday, August 23, 2016

Published August 23, 2016 by with 0 comment

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AIANGUKIA CHADEMA KUHUSU UKUTA,NAO JUMUIYA YA KIKRISTO KUTOA TAMKO KALI,SOMA HAPO KUJUA


 
NA KAROLI VINSENT
MSAJILI wa vya Siasa nchini Jaji Francis Mtungi amekiangukia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pamoja na Chama cha  Mapinduzi (CCM) ambavyo vyama hivyo vilivyopanga kuandamana kwa nyakati tofauti ,kusitisha maandamano hayo.
Amesema wasitishe maandano hayo ili kupisha mazungumzo ambayo yatafanyika kwenye  Baraza la vyama vya siasa ambalo linatarajia kukutana tarehe 29 na tarehe 30 ya  mwezi huu.
Jaji Mtungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari huku akivitaka vyama  hivyo kuacha kufanya maandamano hayo ili suluhu ipatikanekatika baraza hilo.
Amesema Baraza hizo linaloundwa na vyama 20 vilivyopewa usajili litakuwa na lengo la kujadili mambo mbali mbali yanayohusu vyama hivyo.

Kuibuka kwa kauli hii ya msajili wa vyama Siasa nchini inakuja siku moja kupita baada ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) kutangaza kuwa maandamano hayo kuwa yako pale,licha ya kutolewa katazo kutoka jeshi la polisi.
Mbali na Bavicha pia Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM pia nao wametangaza kufanya maandamano kuanzia 31 Agoust mwaka huu kwa kile wanachodai kumpongeza Rais John Magufuli kwa hatua anazofanya.
     JUMUIYA YA WAKRISTO WAJIPANGA KUTOA NENO.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa Fullhabari.blog aliyoko ndani ya jumuiya  ya Kikristo nchini (CCT) ambaye hakutaka kutotajwa jina lake mtandaoni,amesema CCT wanasikitika  na hali ya kisiasa inayotokea nchini huku wakitahadhalisha kuwa nchi kuingia kwenye msuguano.
“Yaani kwa sasa hali inapoelekea nchini ni mbaya sana,yaani kama hawa viongozi wasipoweka tofauti pembeni,basi Taifa litaingia kwenye uhasama ambao unaweza ukarudisha nyuma maendeleo,kwahiyo sisi viongozi wa dini lazima tuibuke na kutoa tamko,kulaani”amesema Mtoa taarifa huyo ambaye pia ni mchungaji wa kanisa moja hapa nchini.
Amesema hatua ya maandamano na mikutano ya hadhara ambayo wanasiasa wanaitaka huku Polisi wakikitaza ,amedai njia hiyo haitaweza kumaliza msuguano huu.
“Sisi viongozi wakiroho hatuwezi tukaa kimya huku Amani ya nchi inaweza ikapoteka kutokana na misuguano hii,lazime tukemee na kuwataka viongozi wamalize misuguano,hata hiyo serikali ya viwanda hawezi kutimia kwa misuguano hii,hapa lazima suluhu ipatikane”ameongeza Kiongozi huyo wa kiroho.
      edit

0 comments:

Post a Comment