Monday, August 22, 2016

Published August 22, 2016 by with 0 comment

Miundombinu duni Soko Kuu la Manispaa ya Songea


Screen Shot 2016-08-22 at 3.45.25 PM
Soko Kuu la Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limelalamikiwa kuwa na miundombinu duni kwa wafanyabiashara na watumiaji wa soko hilo ikiwa ni pamoja na wenye vyombo vya usafiri kukosa mahali pa kuegesha magari yao, hali inayowalazimu kuegesha barabarani na kusababisha kero kwa watumiaji wengine.

Soko hilo limejengwa toka mwaka 2004 eneo lililotengwa kwa ajili ya kuegesha magari ni bovu kiasi cha magari madogo kushindwa kuingia na yakiingia yanatoka kwa tabu, pamoja na miundombinu hiyo mibovu kila gari linatozwa shilingi 500 ushuru wa maegesho hata kama yakiegeshwa barabarani.
Licha ya kero kwa wenye magari watembea kwa miguu nao ni shida kwani maeneo yanayozunguka soko hilo ambalo lipo katikati ya mji makorongo ni mengi,kwa watu wenye ulemavu hulazimika kuchagua maeneo ya kupita ili wafike kwenye maduka ya soko hilo.

Channel ten ilitaka kujua mikakati ya halmashauri ya manispaa ya Songea juu ya ubovu wa miundombinu ya soko kuu inayolalamikiwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa hiyo Tina Sekambo amekili kuwa ni kweli miundombinu sokoni hapo sio rafiki kwa wafanyabiashara na watumiaji wa soko hivyo wataboresha katika bajeti ya fedha ya mwaka huu.
Soko kuu la Manispaa ya Songea liliteketea kwa moto mwaka 2002 lilijengwa upya na kufunguliwa mwaka 2004.

      edit

0 comments:

Post a Comment