Monday, August 22, 2016

Published August 22, 2016 by with 0 comment

BREAKING NEWS,CCM NAO WATANGAZA MAANDAMANO MAKUBWA NCHI NZIMA TAREHE HII HAPA,SOMA HAPO KUJUA


NA KAROLI VINSENT
WAKATI chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikitarajia kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchini nzima kwaanzia tarehe 1 semptemba mwaka huu , kwa kile wanachodai kupinga vitendo vya ukandamizajia kwa vyama vya upinzani vinavyofanywa na Rais John Magufuli.
Nao pia umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)  wametangaza pia kufanya maandaamano nchini nzima siku ya tarehe 31 ya mwezi huu kwa ajili ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kile wanachokisema   hatua “anazochukua Rais huyo kuinua uchumi”.
Shaka Hamdu Shaka ambaye ni  Katibu wa Umoja huo ameyatangaza maandamamo hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari amesema teyari wamemuandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi nchini (IGP)Ernest Mangu wakitaka kuwaruhusu wafanye maandamamo wanayodai ni ya amani.

Amesema katika Barua hiyo yenye Kumbu kumbu namba 40/28/150 ya tarehe 21 mwenzi 8 mwaka huu wamelitaka jeshi hilo litoe kibari cha kufanya maandamano hayo pamoja na kuwapa ulinzi.
Amedai kuwa maandamano hayo yatafanyika nchi nzima na huku Shaka akiwataka viongozi wa UVVCM ngazi ya wilaya kuandaa maandamano hayo.
Hata hivyo,Shaka amesema endapo Jeshi la Polisi likiwanyima kibari cha kufanya maandamano hayo basi wataendelea kufanya maandamano hayo ikiwemo pamoja na kujuilinda wenyewe.
      edit

0 comments:

Post a Comment